Mawaziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kenya Musa Slima na wa Tanzania Samweli Sitta wakitoka kwenye ofisi ya DC Taveta kuhudhuria mkutano wa hadhara uliofanyika Taveta Kenya na kuhudhuliwa na wananchi
wa Tanzania na Kenya.
-----------------------------------------------------------
Serikali za Tanzania
na Kenya zimetangaza hatua kadhaa za kuwawezesha wafanyabiashara wadogo wa
mipakani mwa nchi hizo kuingia katika nchi nyingine kufanya biashara bila hati
ya kusafiria na wakuu wa wilaya za mipakani wameagizwa kukaa pamoja na kuandaa
utaratibu utakaotumika.
Makubaliano
hayo yamefikiwa katika wilaya ya Taveta nchini kenya na kusainiwa na mawaziri
wa jumuia ya afrika mashariki Bw Samwel Sita wa Tanzania na Musa Srima wa Kenya
mbele ya wananchi wa pande zote hizo katika mkutano wa hadhara ambao viongozi
hao walitoa ufafanuzi juu ya hatua hizo.
Waziri Sita amezitaja baadhi ya hatua hizo kuwa na
fomu maalum za kuwatambulisha wafanyabiashara hao kufanya biashara zao katika
masoko ya jirani yaliyo ndani ya umbali wa kilomita 20 kati ya nchi na nchi
wakiwemo waendesha pikipiki. Akitoa ufafanuzi waziri Srima amesema, katika
makubaliano hayo maafisa forodha wa pande zote wametakiwa kutoa elimu ya
kutosha kwa wafanyabiashara wakubwa ya namna uvushaji na ulipaji wa ushuru wa
bidhaa zao na kuangalia uwezekano wa kufanya kazi kwa saa 24 wa idara zzote
zikiwemo za uhamiaji.
Chanzo:Picha na Habari na Dixon Busagaga
wa Globu ya Jamii, Moshi.
0 comments:
Post a Comment